poslat odkaz na aplikaci

Biblia Takatifu - Biblia Kiswahili (The Bible in Swahili)


4.0 ( 4000 ratings )
Manuály Vzdělávání
Vývojář: Stratagem PM
1.99 USD

Programu-tumizi hii ya Biblia ina mistari,sura na vitabu vya Biblia. Tumehusisha vipengele vingi kuboresha kusoma kwako kwa Biblia.
Kutafuta
Unaweza kutumia kisaidizi katika programu-tafiti hii kukusaidia kupata mistari ya Biblia inayohusu mada tofauti tofauti. Kwa urahisi, unaandika unalolitafuta na programu-tumizi hii itakupa mistari inayolingana na uliloandika.
Shrikisha marafiki kupitia Facebook, Twitter na barua pepe.
Unaweza kuwatumia watu mistari ya Biblia kupitia Facebook, Twitter ama barua pepe ( na pia kutoa maoni yako kama ungependa).
Andika maombi na fikra
Watumizi wetu wengi waliulizia kifaa ambacho wangeweza kuandika maombi, fikra ama ufunuo wanazopata wanaposoma Biblia. Sasa, kwa programu-tumizi hii, unaweza kuandika maombi na fikra zako, uzihifadhi na kuwatumia marafiki wako kwa Facebook, Twitter ama barua pepe.
Weka alama bainishi kwa mistari ya Biblia
Unaweza kuangazia mistari tofauti ya Biblia na rangi unayoipenda. Kwa urahisi, tumia kipanya chako kubonyeza ikoni ya penseli kwa sehemu ya juu ya skrini yako unaposoma Biblia na kuangazia kwa rangi mstari unaotaka.
Alamisho
Alamisho linakusaidia kuweka alama kwa mistari tofauti unayosoma. Ikoni hii iko sehemu ya juu ya skrini yako. Kwa kutumia kipanya chako, utabonyeza ikoni hii. Ukirudi kutumia programu-tumizi hii, utabonyeza ikoni hii tena na utarudishwa ulipoachia.
Tafuta na ulinganishe mistari ya Biblia (katika programu-tumizi hii)
Programu-tumizi hii ina kifaa-kisaidizi kinachogawanya skrini yako kwa sehemu mbili. Kwa hivyo, utaweza kuitazama mistari miwili ya Biblia zikiwa zimepakiana upande kwa upande.

Kifaa cha kujifunza
Unaweza kutengeza waraka ya mstari au mistari ya Biblia. Hili utafanya kwa kudokeza kando ya mistari unayosema. Ukishamaliza kuandika waraka hii, unaweza kuituma kwa watu ukitumia barua pepe kupitia programu-tumizi hii.
Toleo la ‘King James’ la Kiingereza
Soma toleo la King James la Biblia kwa lugha ya Kiingereza. Linganisha mistari kutoka Biblia la Kiswahili na ile ya Biblia hii ya Kiingereza.
Wasiliana nasi
Tunakaribisha maoni yako. Tutakusikiza na kusahihisha programu-tumizi hii kulingana na maoni yako. Unaweza kutumia ujumbe kupitia kifaa cha Wasiliana Nasi katika programu-tumizi hii.